Julai 9, 2024 saa tatu asubuhi kwa saa New York Marekeni, Kampuni ya NALA iliyoanzishwa na Kijana Mtanzania Benjamin Fernandes, imetangazwa kwenye soko la hisa la Marekani NASDAQ kupata uwekezaji wa dola za Kimarekani milioni 40 ( Tsh. Bilioni 106) uwekezaji ambao utaiwezesha kutimiza lengo lake la kukua zaidi kimataifa na kuboresha ubora na usalama wa malipo barani Afrika kwa kupita mfumo mpya wa malipo uliotengenezwa na Kampuni hiyo uitwao Rafiki.
NALA imepata uwekezaji huu kutoka kwenye Kampuni kubwa za Uwekezaji duniani kama vile Acrew Capital, DST Global, Amplo na nyinginezo ambapo itatumia uwekezaji huu kutimiza malengo yake ya kimataifa kwa kufanya vitu vikuu viwili kwa sasa ambavyo ni kuongeza huduma za kutuma na kupokea fedha nje ya Afrika na kutengeneza huduma za kibenki kwa ajili ya Wahamiaji na Watu waishio ughaibuni.
Taarifa ya NALA imesema mfumo wake mpya wa kimataifa wa malipo uitwao Rafiki unatarajiwa kutumiwa na Watu Bilioni ambapo utawahakikishia Wateja huduma za malipo zenye ubora na usalama wa kiwango cha juu, huduma nzuri za fedha za kigeni, gharama nafuu za miamala na kuwezesha biashara kutuma na kupokea malipo kwa urahisi sambamba na kuleta mapinduzi kwenye huduma za malipo barani Afrika kama yale yaliyofanywa na kampuni ya dlocal Amerika kusini pamoja na AirWallex huko barani la Asia.
NALA imeendelea kufanya vizuri zaidi kwa miezi 12 iliyopita na kushuhudia idadi ya miamala inayochakatwa kwenye NALA ikiongezeka mara 34 zaidi, idadi ya Wafanyakazi ikiongezeka kutoka watu 7 hadi 100 huku idadi ya Wateja ikifikia Watu laki 5 na kuongeza Matawi kwenye nchi 21 za Ulaya. Benjamin akiongea na millard ayo amesema yafuatayo “Uwekezaji huu wa Bilioni 106 utatuwezesha kuongeza huduma zetu za kifedha, yaani mbali na kutoa huduma za remittances (kutuma fedha kutoka ughaibuni kwenda nyumbani Afrika) tutatoa huduma mpya za malipo za kimataifa nje ya Afrika, tutatumia hii pesa kuboresha miundombinu ya mfumo wetu mpya wa malipo (uitwao Rafiki), kuboresha ubora na uharaka wa huduma za kifedha pamoja kupunguza gharama za miamala, NALA hatushiriki tu kwenye mabadiliko ya huduma za kifedha ila sisi ndio tunafanya hayo mabadiliko" . . .
#ramado1.com #Ramado1Radio #Ramado1MediaUPdates Source @millard ayo